Ukurasa wa mwanzo - Video - Ujumbe wa Video wa Chini ya Ufuniko

 
Ujumbe wa Video wa Chini ya Ufuniko
Ujumbe wa Video wa Chini ya Ufuniko
Mwalimu: John Bevere

Chini ya uvuli wake Mwenyezi, kuna uhuru, upaji, na ulinzi. Kwa bahati mbaya, wengi hawaelewi jinsi ya kupapata mahali hapa pa siri. Badala yake wanalaghaiwa waamini uhuru wa kweli wenye kudumu unaweza kupatikana nje ya mamlaka ya kimungu.

Katika chini ya Ufuniko, John Bevere anazifichua mbinu za kijanja ambazo anazitumia adui, akitufanya sisi tushindwe kutambua na kuhusiana ipasavyo na mamlaka ya kimungu. Kwa mifano ya kiutendaji na msingi imara wa kibiblia, ujumbe huu unatukumbusha kwamba ufalme wa Mungu ndivyo vivyo hivyo ulivyo: ufalme, unatawaliwa na Mfalme, ambapo kuna utaratibu na mamlaka.

Unapoikumbatia kweli ya Neno la Mungu, utajifunza jinsi ya kuitikia kutendewa kwa haki na kusiko sawa. Utagundua tofauti kati ya unyenyekevu wa kweli wa kibiblia na utii, na utakua katika ufahamu wa kusudi la Mungu la mamlaka. Ujumbe huu utakuweka katika nafasi ya kutembea katika utimilifu na tabia ya Mungu.

Shiriki kwenye mtandao wa