Ukurasa wa mwanzo - Video - Kuua Kidhoofishacho wa Mtaala kwa Video

 
Kuua Kidhoofishacho wa Mtaala kwa Video
Mwalimu: John Bevere

Unaweza Kuangamiza Kinachoiba Nguvu Zako

Jinsi ilivyo na Superman anayeweza kuruka juu ya kizuizi chochote na kumshinda adui yeyote, wafuasi wa Kristo wana uwezo wa kiungu wa kushinda changamoto zozote tunazokabiliana nazo. Lakini shida iliyoko kwa Superman na kwetu pia ni kwamba kuna kidhoofishi (kryptonite) kinachoiba nguvu zetu.

Bila shaka, Superman na kryptonite ni dhana bunifu. Lakini kidhoofishi cha kiroho si bunifu.

Kitabu hiki kinatoa majibu ya ni kwa nini wengi wetu hukosa kuwa na uzoefu wa kutembea katika nguvu za kiungu zilizokuwa dhahiri kati ya wafuasi wa Kristo wa karne ya kwanza.

Katika Kuua Kidhoofishacho, John Bevere anaweka wazi kidhoofishi hiki ni nini, ni kwa nini kinazuia jamii zetu zisifikie upeo wa uwezo zilizo nazo, na jinsi ya kuwekwa huru kutoka kwa kifungo chake.

Kitabu Kuua Kidhoofishacho si kwa wenye moyo dhaifu; si kitamu cha kusisimua na kufurahisha tu. Huu ni ukweli madhubuti kwa mfuasi yeyote wa Kristo anayetamani kuichukua njia iliyo na changamoto lakini pia na thawabu za mabadiliko maishani mwake.

Rasilimali katika familia moja:
Kuua Kidhoofishacho
Kuua Kidhoofishacho wa Mtaala kwa Audio
Kuua Kidhoofishacho – Kitabu cha Kusikilizwa

Shiriki kwenye mtandao wa