Ukurasa wa mwanzo - Vitabu - Hadithi ya Ndoa

Hadithi ya Ndoa
Mwalimu: John Bevere

Hapo zamani za kale… Ndoa ilikuwa idumu milele. Ilikuwa agano lililomuunganisha mwanaume mmoja na mwanamke mmoja. Mwungano huu ulifanya kila mmoja wao awe na nguvu zaidi, bora zaidi na awe dhihirisho bora zaidi wa kile alichoumbwa na Mungu kuwa. Walifanyika bora zaidi kwa kuwa pamoja kuliko jinsi walivyokuwa walipokuwa watu binafsi. Harusi ilikuwa ni mwanzo tu. Ilikuwa ni lango la kuwawezesha kuingia kipindi cha kujenga “raha mustarehe milele” ya kivyao. Maamuzi na matendo yao yote yalikusudiwa kujenga maisha yaliyowakilishwa na mwungano wao. Mume na mke walikuwa wakitembea na kuingia kwenye sintofahamu kuu iliyokuwa mbele yao pamoja, wakiwa na mioyo, mikono, na sauti zilizounganika kudhihirisha upendo wa Muumba wao.

Tulipotezaje ufahamu wa hadithi hii ya upendo wa kina kikuu hivi? Katika Hadithi ya Ndoa, John na Lisa Bevere wanakukaribisha kuugundua tena mpango asili wa Mungu. Haijalishi kama tayari umekwisha funga ndoa, hujaoa au kuolewa, au una mchumba, hadithi yako ni sehemu ya hadithi Yake Mungu.

Nakili-chukua (~3.19 MB)

Shiriki kwenye mtandao wa