Ukurasa wa mwanzo - Kwa kusikiliza - Mungu, Uko Wapi?! – Kitabu cha Kusikilizwa

 
Mungu, Uko Wapi?! – Kitabu cha Kusikilizwa
Mwalimu: John Bevere

Kupata Nguvu na Kusudi Katika Jangwa Lako

Je, unahisi ni kana kwamba umepoteza mwelekeo ndani ya msimu mgumu na unajiuliza, “MUNGU, UKO WAPI?!”

Pengine ulimsikia Mungu akikuzungumzia, lakini sasa ni kama amekimya. Labda ulipiga hatua za kwenda mbele kwa imani, lakini sasa huuhisi uwepo wake tena. Karibu jangwani–mahali pa katikati kati ya kupewa ahadi kutoka kwa Mungu na kuiona ikitimia.

Lakini kuna habari njema, nayo ndio hii–hili sio jangwa lisilo na kusudi maalum. Mungu hutumia kipindi cha kuwa jangwani kukuandaa na kukupa vifaa vya kutimiza hatma yako–ukipita humo jinsi inavyostahili. Kinyume na vile watu wengi wanavyofikiria, kuupitia msimu huu sio swala la kumngojea Mungu tu. Una jukumu la kutekeleza katika safari yako humo. Na ni jukumu kubwa. Na kama hutaki kupoteza wakati ukizungukazunguka humo bure, ni muhimu kujifunza jukumu hilo ni lipi.

Katika kitabu hiki cha kufumbua macho, mwandishi mashuhuri John Bevere anakupa vifaa muhimu vya ufahamu kutoka kwa Biblia na hadithi za kina zitakazokusaidia kupitia misimu yako ya ukame au ugumu na hatimaye kuingia katika yote uliyotayarishiwa na Mungu.

Pakua faili zote (ZIP): ~315.68 MB

Rasilimali katika familia moja:
Mungu, Uko Wapi?!
Mungu, Uko Wapi?! wa Mtaala kwa Video
Mungu, Uko Wapi?! wa Mtaala kwa Audio

Shiriki kwenye mtandao wa