Ukurasa wa mwanzo - Kwa kusikiliza - Msukumo wa Enzi ya Milele wa Mtaala kwa Audio

 
Msukumo wa Enzi ya Milele wa Mtaala kwa Audio
Mwalimu: John Bevere

Maisha haya hapa duniani ni mvuke tu, lakini bado wengi wetu huishi kana kwamba hakuna chochote upande ule mwingine wa kifo. Ukweli ni kwamba jinsi tutakavyoishi milele kunategemea jinsi tunavyoishi sasa. Maandiko yanatwambia kutakuwa na viwango mbali mbali vya thawabu kwa waumini–kutoka kutazama yote tuliyoyafanya yakiteketezwa hukumuni, hadi kuwa na fursa ya kutawala na Kristo Mwenyewe.

Akitumia kanuni kutoka 2 Wakorintho 5:9-11, John Bevere anatukumbusha kwamba waumini wote watasimama mbele ya Kristo kupokea malipo ya waliyoyafanya maishani mwao. Wengi wetu watastaajabu kugundua kwamba wingi wa wakati wetu ulitumika kufanya vitu ambavyo havikustahili thawabu za milele.

Kwa hivyo tunawezaje kuyaendeleza maisha yatakayoacha alama ya kudumu? Katika Msukumo wa Enzi ya Milele, utajifunza jinsi unavyoweza kugundua mwito wako na jinsi ya kuzidisha kile ulichopatiwa na Mungu. Unapopata kuyaangalia mambo kutoka kwa mtizamo wa milele, utatiwa nguvu kufanya kazi kwa ajili ya kile kitakachodumu milele.

Rasilimali katika familia moja:
Msukumo wa Enzi ya Milele
Msukumo wa Enzi ya Milele wa Mtaala kwa Video
Msukumo wa Enzi ya Milele – Kitabu cha Kusikilizwa

Shiriki kwenye mtandao wa