Ukurasa wa mwanzo - Kwa kusikiliza - Afabeli

 
Afabeli
Mwalimu: John Bevere

Umechukua muda kuufikiria umilele? Waweza kuwa unajua utaishi wapi milele, lakini unajua utaishije wakati huo?

Ni muhimu kwa waumini kuishi wakiwa na mtizamo wa enzi ya milele, lakini umilele unaweza kuwa mgumu kuelewa. Mchezo huu wa kuigiza wa kusikilizwa ulioandikwa kwa ufasaha mkubwa kutoka kwa kitabu Msukumo wa Enzi ya Milele kilichoandikwa na John Bevere unatupatia dirisha la kuona ni kipi kilichoko baada ya maisha ya hapa duniani.

Jiunge na Mfalme mwenye Enzi Jalini, bwana wa giza Dagoni, Pendo, Kivyake na wengine unapotembelea nchi ya ajabu ya Afabeli, na sehemu za nje za kuogofya za nchi ya Upweke. Maisha yako yatabadilishwa waigizaji hawa wanapoyadhihirisha yaliyo moyoni mwako.

Shiriki kwenye mtandao wa