Lugha inayotumika sasa: sw Kiswahili

Lugha
Selected Language:

Ukurasa wa mwanzo - Kuhusu

Kuhusu Maktaba ya Cloud

Messenger International ina lengo wakfu kwa ulimwengu mzima la kuzifanya raslimali hizi zipatikane kwa wachungaji na viongozi bila ya kujali mahali au ngazi ya kifedha. Maktaba ya Cloud ilitengenezwa kwa ajili ya kusudi hilo. Inahudumu kama chanja ya kusambaza ya kimataifa ambayo inaruhusu raslimali zilizotafsiriwa zionyeshwe na kunakiliwa na kuchukuliwa bure.

Lengo letu ni kuzifanya raslimali hizi kupatikana kwa kila lugha iliyo kubwa, kwa jinsi hiyo kuwa na uwezo wa kufikia zaidi ya 98% za idadi ya watu duniani. Maktaba ya Cloud ni njia moja ya kulitekeleza lengo hili. Kwa nini, wauliza? Kwa sababu raslimali zizalishwazo kwa kompyuta zinaweza kuzidika na kusafiri kwa haraka zaidi kuliko raslimali za asili. Twatumainia utaufurahia uzoefu wako ndani ya Cloud.

Kutoka kwa Waanzilishaji

Yesu ametuagiza si tu tuhubiri injili, lakini pia tukuze wanafaunzi. Jumbe hizi zitakusaidia kuwa mwanafunzi wa Kristo. Tunawekeza katika mafunzo yako kwa sababu tunakwamini wewe na uwezo wako, kwa neema ya Mungu, uubadilishe ulimwengu wako wa ushawishi. Mungu ameweka ukuu ndani yako, na ana shauku ya kukujua wewe kwa karibu sana. Raslimali hizi zitakusaidia kugundua uhusiano na Mungu wa karibu na ulio binafsi. Unapokua katika uhusiano wako na Kristo, utabadilishwa kwa uweza wa Neno Lake.

Mungu amekuumba kwa kusudi ambalo ni la kipekee kufuatana na karama zako na ushawishi. Tunakutia moyo utafute utimilifu wa kila kitu alichonacho Mungu kwa ajili yako. Maombi yetu ni ya kwamba raslimali hizi zikuandae katika safari yako ya ugunduzi.

Baraka ziwe juu yako na ni wako,

John & Lisa Bevere

Yafadhili Maono

Je! moyo wako unawaka uzione raslimali zenye kubadilisha maisha zinagawanywa katika ulimwengu mzima? Ikiwa unapendezewa na kuufadhili umisheni wa Maktaba ya Cloud, tafadhali email getinvolved@cloudlibrary.org. Tunakushukuru kabla kwa maombi yako na ufadhili!